Unawezaje kuandaa mashairi yako na kutengeneza ushairi wako kibunifu?
Ninaweza kufanya hivyo kupitia hamasa na msukumo ninaopata kutoka kwenye maisha ya watu wanaonizunguka, kupitia kazi za uandishi za washairi na watunzi mbalimbali, kupitia habari mbalimbali zinazojiri mitandaoni na duniani kwa ujumla na kupitia sanaa nyingine kama maigizo na filamu, michezo (dance), picha na uchoraji, Muziki na nyimbo n.k. Msukumo au hamasa hiyo ndiyo hunipa hisia stahili ambayo ndiyo nitaitumia kutengeneza wazo nitakaloliandikia. Hata hivyo, Mara chache huwa naandaa mashairi yangu kwa kujipa au kupewa changamoto ya mada inayohitaji utunzi wa namna fulani.